Malkia Strikers waambulia kichapo cha pili Olimpiki

Dismas Otuke
1 Min Read

Matumaini ya timu ya Kenya ya Voliboli ya wanawake kuzoa angaa seti katika michezo ya Olimpiki ya Paris, yalitumbukia nyongo Jumatano, baada ya kucharazwa seti 3-0 na Poland katika mechi ya pili kundini B.

Kenya walianza vibaya  mechi hiyo ya Jumatano usiku wakipoteza ,pointi 14-25 ,lakini wakajizatiti ya pili ingawa walipoteza 17-25 na  na 16-125 katika seti ya mwisho.

Matokeo hayo yalikuwa nafuu baada ya kushindwa mechi ya kwanza dhidi ya Brazil kwa seti za 14-25,13-25 na 12-25.

Ushinde huo ulikuwa wa pili mtawalia kwa Kenya wakipoteza seti 3-0 katika  mechi ya ufunguzi dhidi ya Brazil.

Kenya inayofunzwa na kocha Japheth Munala itarejea uwanjani Jumamosi hii kwa mechi ya mwisho dhidi ya Japan.

Share This Article