Mali wafuzu mashindano ya Olimpiki soka la wanaume

Dismas Otuke
1 Min Read
Cheickna Diakite of Mali and Fode Doucoure of Mali and Alkalifa Coulibaly of Mali celebrates victory during the 2023 U23 Africa Cup of Nations 3rd place match between Mali v Guinea held at Ibn Batouta Stadium in Tangier, Morocco on 07 July 2023 © Ladjal Djaffar/BackpagePix

Timu ya taifa ya Mali maarufu kama the Flying Eagles, imejikatika tiketi kushiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao jijini Paris, Ufaransa baada ya kuwalemea Guinea mabao 4-3 kupitia penati kufuati sare kappa .

Mechi hiyo iliyochezwa ijumaa kiwarani Ibn Batouta mjini Tangier Ijumaa usiku ,ilishuhudia timu zote zikibuni nafasi haba za kufunga mabao na kulazimu penati zipigwe kutenganmisha ngano na makappi.

Guinea walifunga penati 3 huku moja ikipanguliwa na kipa wa Mali huku nyingine ikipigwa nje.

Mchuano huo ulihudhuria na maafisa wa baraza kuu la shirikisho la kandanda Afrika wakiongozwa na kinara Dkt, Patrice Motsepe na magwiji wa soka waliostaafu.

Fainali ya makala ya mwaka huu ambayo ni ya tatu na yanayoandaliwa nchini Morocco kwa mara ya pili tangu mwaka 2011 itasakatwa Jumamosi usiku katika uga wa Prince Mouley Abdellah jijini Rabat ,kati ya wenyeji Atlas Lions dhidi ya mabingwa watetezi Misri.

Misri na Morocco tayari pia wamewahi tiketi ya kushiriki Olimpiki.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *