Msanii wa Muziki kutoka Tanzania, Malaika Gray, amesaini mkataba na Kampuni ya Africori, iliyo chini ya Warner Music Group ikiwa ni hatua muhimu katika safari yake ya muziki kuelekea Soko la Kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 15, 2026, Malaika anatarajiwa kutoa wimbo wake wa kwanza unaoitwa My Fever, aliomshirikisha Msanii wa Bongo Fleva, Marioo, Oktoba 30, 2026.
Wimbo huo umeandikwa kwa ushirikiano wa Malaika na Marioo, huku utayarishaji wake ukifanywa na Producer Abbah Process ukichanganya mitindo ya Afrobeats, Bongo Fleva, R&B na Pop.
Video ya wimbo huo iliongozwa na Joma na kurekodiwa katika maeneo mbalimbali ya Dar es salaam.
Wasanii wengine wa Tanzania walio kwenye mikataba na kampuni hiyo ya Africori chini ya Warner Music Group ni pamoja na Diamond Platnumz na Juma Jux.