Makumi ya maelfu ya waandamanaji walijitokeza katika maaandamano ya Jumamosi katika mji mkuu wa Ufaransa Paris.
Maandamano hayo ni ya hivi punde ikiwa miezi mitatu tangu maandamano mengine yaliyoponga mauaji ya kijana mmoja aliyepigwa na polisi barabarabni.
Waandamanaji walipinga mauaji ya kiholela ya polisi wakibeba mabango ya kuwataka poliso kukomesha unyama huo dhidi ya raia.
Maandamano hayo pia yaliandaliwa katika maeneo mengi nchini Ufaransa ikikisiwa kuwa watu 80,000 walishiriki wakiwemo 9,000 walijitokeza katika mji mkuu.