Katibu katika Wizara ya Fedha Dkt. Chris Kiptoo sasa anawataka maafisa wa uhasibu serikalini kuangazia changamoto ya madeni anayosema yanaathiri uchumi kwa njia hasi.
Dkt. Kiptoo anasema kamati baina ya wizara iliyoundwa kuangazia suala hilo itakutana tena katika kipindi cha miezi miwili ijayo kuakisi hatua iliyopigwa katika ulipaji wa madeni hayo yanayozidi shilingi bilioni 300 billion.
Makatibu wa Wizara walio na miradi iliyokwama kwa upande mwingine wametakiwa kushirikiana na mamlaka husika kuhakikisha miradi mbalimbali inatekelezwa.
Mnamo mwezi Februari mwaka huu, bunge lilianzisha uchunguzi wa madai ya kuchepuliwa kwa fedha zilizokusudiwa kuwalipa wasambazaji bidhaa na watoa huduma madeni yao ambayo yalikuwa shilingi bilioni 646.8 mwezi Disemba mwaka jana.