Makatibu wa Wizara wahaha kufuatia tangazo la kuwaajiri Makatibu wapya

Dismas Otuke
1 Min Read
Tume ya utumishi wa umma,PSC

Mabadiliko ya Makatibu wa Wizara yanatarajiwa hivi karibuni kufuatia tangazo la serikali la kuwaajiri Makatibu wapya mapema wiki hii .

Mabadiliko hayo yamekuwa yakinukia hususan tangu kubadilishwa kwa Mawaziri kwenye wizara mbalimbali, kufuatia maandandano ya vijana mwezi Juni.

Ingawa tangazo hilo la makatibu liliashiria nafasi moja, fununu za kuaminika zinaashiria takriban Makatibu wote wa sasa 36 wataathiriwa aidha kwa kuhamishwa au kufurushwa afisini.

Mabadiliko hayo yanatarajiwa kuambatana na mfumo mpya wa serikali jumuishi iliyobuniwa ikijumuisha upinzani.

Yamkini tanganzo hilo limewanyima Makatibu wa sasa usingizi wengi wao wakihofia kuwa kazi zao zitaota nyasi.

Share This Article