Hatima ya Makamu wa Rais wa Malawi Dkt. Saolus Claus Chilima haijulikani baada ya ndege ya kijeshi aliyokuwa akisafiria mapema Jumatatu kutoweka angani.
Taarifa kutoka kwa Ikulu ya Rais Lazurus Chakwera imesema kuwa ndege hiyo iliondoka Lilongwe saa tatu na dakika 17 asubuhi, na ilitarajiwa kutua katika uwanja wa Mzuzu saa nne na dakika mbili ,hali ambayo haikutokea.
Rais ameaihirisha ziara yake nchini Bahamas na kuwaamrisha wanajeshi kutafuta ndege hiyo.
Ndege hiyo ilipotea kwenye mitambo ya rada ikiwa angani na ilikuwa imembeba Makamu wa Rais pamoja na watu wengine tisa ilipotoweka