Makala ya kwanza ya kipute cha ligi mpya ya Afrika, AFL kuanza Oktoba 20

Dismas Otuke
2 Min Read

Ligi mpya ya Afrika baina ya vilabu maarufu kama African Football League, AFL itang’oa nanga Oktoba 20 jijini Dare Salaam, Tanzania kulingana na shirikisho la kandanda barani Afrika, CAF.

Ligi hiyo itashirikisha vlabu vinane katika makala hayo ya kwanza kabla ya timu kuongezwa hadi 24 msimu wa mwaka 2023/2024.

AFL ni ligi ambayo imezinduliwa kwa ushirikiano wa CAF na shirikisho la soka ulimwenguni, FIFA na makala ya kwanza yanashirikisha vlabu kutoka kanda za Afrika Magharibi, Magharibi na Kati na Kusini Mashariki mwa Afrika.

Ukanda wa kaskazini mwa Afrika utawakilishwa na timu za Al Ahly ya Misri, Espérance Sportive de Tunis ya Tunisia na Wydad Athletic Club ya Morocco.

Kutoka magharibi na katikati mwa Afrika, kutakuwa na Enyimba ya Nigeria na Tout Puissant Mazembe na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini,  Atlético Petróleos de Luanda ya Angola na Simba Sports Club kutoka Tanzania ya Afrika mashariki.

Droo ya makala hayo itaandaliwa jijini Cairo nchini Misri mnamo Septemba 2 huku mechi ya kwanza ya robo fainali ikichezwa jijini Dares-Salaam, Tanzania Oktoba 20.

Timu zitacheza mechi za nyumbani na ugenini huku nusu fainali zikipigwa baina ya Oktoba 29 na Novemba mosi kisha mkondo wa kwanza wa semi fainali uandaliwe Novemba 5 na marudio tarehe 11 mwezi Novemba.

Website |  + posts
Share This Article