Mahakama zaandaa shughuli za kuzindua mwezi wa huduma kwa watoto

Marion Bosire
1 Min Read

Vituo mbali mbali vya mahakama nchini vimeandaa shughuli za kufana za kuzindua mwezi wa huduma kwa watoto.

Idara ya mahakama ilitenga mwezi Novemba kuwa mwezi wa huduma kwa watoto ili kutoa kipaumbele kwa kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi zote zinazohusu watoto nchini.

Vituo vilivyoandaa shughuli hizo ni pamoja na Wang’uru, Makindu, Kajiado, Engineer, Othaya na Gichugu.

Mwaka 2016, baraza la kitaifa la utekelezaji haki almaarufu National Council on Administration of Justice, lilizindua jopokazi maalumu la masuala ya watoto, kupitia kwa gazeti rasmi la serikali chapisho nambari 369 la Januari, 29,.

Wanachama wa jopokazi hilo ni wawakilishi wa mashirika mbali mbali ikiwemo idara ya mahakama, magereza, chama cha wanasheria, idara ya upelelezi wa jinai kati ya mengine mengi.

Baraza la utekelezaji haki lilichagua mwezi Novemba kwa sababu ni mwezi wa maana kwa masuala ya haki za watoto kutokana na ukweli kwamba baraza kuu la umoja wa mataifa liliidhinisha mkataba wa UNCRC Novemba 20, 1989.

Mkataba huo ndio ulibuni shirika la umoja wa mataifa la kushughulikia haki za watoto UNICEF.

Share This Article