Mahakama yaongeza muda wa maagizo ya kusimamisha sheria ya fedha

Tom Mathinji
1 Min Read

Mahakama kuu imeongeza muda wa maagizo ya kusimamisha utekelezaji sheria ya fedha ya mwaka 2023 hadi Jumatatu wiki ijayo.

Jaji Mugure Thande ataamua siku hiyo ikiwa ataongeza muda zaidi wa maagizo hayo, kusubiri kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi hiyo.

Juma lililopita, mahakama kuu ilisimamisha kwa muda kutekelezwa kwa sheria hiyo, hadi kesi iliyowasilishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Omtatah na mwanasheria Otiende Omollo kwenye mawasilisho yao, waliitaka mahakama kudumisha maagizo yaliyotolewa Ijumaa wiki iliyopita.

Kwenye uamuzi wake Jumatano alasiri, jaji Thande aliongeza maagizo hayo kwa siku tano zaidi hadi siku ya Jumatatu, Julai 10, 2023 wakati kesi iliyowasilishwa na seneta Omtatah itasikilizwa.

Seneta huyo anapinga utekelezaji wa sheria ya kifedha kwa msingi kwamba bunge la seneti halikushirikishwa katika kupitishwa kwa sheria hiyo tata.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *