Mahakama ya rufaa ya Kenya imekataa kuzuia kurejeshwa nchini Zanzibar kwa shehena ya mpunga feki,uliokuwa umewasilishwa humu nchini.
Majaji Stephen Kairu, Agnes Murgor, na Kibaya Laibuta pia walikatalia mbali ombi mshtaki kwenye kesi hiyo aliyetaka arejeshewe shilingi bilioni 3.2 , alizotoa kama faini alipoongiza shehena hiyo ya mpunga humu nchini.
Mahaka ya rufaailibatilisha uamuzi wa mahakama kuu katika kesi ya mamlaka ya ushuru nchini KRA, uliotaka mwagizaji wa shehena hiyo arejeshewe pesa zake .
Mounga huo ulipatikana kuwa usiofaa kwa matumizi .