Mahakama ya kikatiba nchini Msumbiji imeidhinisha ushindi wa Danie Chapo kuwa Rais wa taifa hilo baada ya kukumbwa na machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu.
Mahakama hiyo imemthibitisha Chapo wa Chama cha Mozambique Liberation Front (Frelimo) kuwa mshindi baada ya kuzoa asilimia 65.17.
Chapo aliye na umri wa miaka 47 ataapishwa mwezi ujao huku akihudumu afisini kwa kipindi cha miaka mitano akiwa Rais wa tano.
Vyama vya upinzani pamoja na makundi ya wanaharakati wamekuwa wakiandaa maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi huo wa Oktoba 9.