Mahakama yazuia SRC kusitisha marupurupu ya wauguzi

Dismas Otuke
1 Min Read

Ni afueni kwa wauguzi kote nchini baada ya Mahakama ya Leba kuizuia tume ya kuratibu mishahara ya watumishi wa umma, SRC kuondoa marupurupu ya utendakazi ya wauguzi ambayo wamekuwa wakipokea.

SRC ilitaka kuondoa marupuru hayo kwa wauguzi wasiofanya kazi katika hospitali za umma.

Hatua hiyo ilipingwa vikali na chama cha madaktari nchini, KMPDU na kuhiari kuelekea mahakamani kutafuta haki.

KPMDU wamesimama kidete kuwa wauguzi walio katika sekta za kibinafsi na wale wa umma wanastahiki kuendelea kufurahia marupurupu hayo.

TAGGED:
Share This Article