Mahakama ya Korea Kusini yaamuru kukamatwa na kushtakiwa kwa Yoon Suk Yeol

Dismas Otuke
1 Min Read

Mahakama ya Korea Kusini imeamuru kukamatwa na kushtakiwa kwa Rais Yoon Suk Yeol aliyeng’olewa mamlakani na bunge kwa kukiuka sheria alipowaamuru wanajeshi kuwavamia raia.

Itakuwa mara ya kwanza kwa Rais aliye afisini kukamatwa na kushtakiwa nchini Korea Kusini.

Yoon alibanduliwa mamlakani baada ya wabunge kupiga kura ya kukosa imani naye huku pia Waziri Mkuu Han Duck-soo, aliyeteuliwa kuwa Kaimu Rais, akifurushwa na wabunge wiki jana.

Waziri wa Fedha Choi Sang-mok ndiye kaimu Rais kwa sasa, huku akikabiliana na kibarua cha kubaini chanzo cha ajali mbaya ya ndege iliyotokea Jumapili iliyopita na kusababisha vifo vya watu 179.

Kibali cha kukamatwa kwa Yoon kitadumu hadi Januari 6 na punde atakapotiwa mbaroni atawekwa kizuizini mjini
Seoul.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *