Mahakama Kuu imetanga Juni 6 mwaka huu, kama siku ya kutoa uamuzi kuhusu kesi inayotaka mwili wa marehemu Rais mstaafu Mwaki Kibaki ufukuliwe ili kufanyiwa utathmini wa msimbojeni wa DNA.
Jacob Ochola mwanamke anayejiita JNL walienda kotini wakitaka mgao wa mali ya hayati Rais mstaafu Kibaki, wakidai kuwa watoto wake na wameomba mahakama kuamrisha kufukuliwa kwa mwili ili kufanyiwa uchunguzi wa DNA.
Wawili hao pia wanataka kutambuliwa kama watoto wa marehemu Kibaki na kupewa urithi.
Katika kesi ya kwanza wawili wameiomba mahakama kuamrisha uchunguzi wa DNA kwa watoto wanne wa Kibaki ambao ni-
Judy, James Mark Kibaki, David Kagai Kibaki na Anthony Andrew Githinji Kibaki.
Kesi ya pili ya wawili hao wanataka mahakama kuamrisha kufukuliwa kwa mili wa kibaki na kuchunguzwa DNA.
Hata hivyo familia ya Kibaki kupitia kwa wakili wao wametaka muda zaidi ili kuandaa ushahidi dhidi ya kesi hiyo.