Magavana waitisha kikao cha dharura kufuatia changamoto za fedha

Martin Mwanje
1 Min Read
Ahmed Abdullahi - Mwenyekiti wa Baraza la Magavana

Baraza la Magavana (CoG) limeitisha kikao cha dharura keshokutwa Ijumaa ili kujadili masuala mbalimbali yanayoathiri utendakazi wa serikali za kaunti ikiwa ni pamoja na  kupunguzwa kwa bajeti kwa takriban shilingi bilioni 25.

Magavana hao wanamtaka Waziri wa Fedha John Mbadi kutoa maelezo ya ni kwa nini  ratiba ya bajeti ya miradi inayofadhiliwa na wafadhili imepunguzwa kwa kiwango kikubwa.

CoG inayoongozwa na Gavana wa Wajir Ahmed Abdullahi sasa inalishikiza Bunge la Seneti kukataa katakata hatua ya kupunguza bajeti hiyo.

Abdulahi amesema kuwa mkataba wa pekee baina ya baraza hilo na wabunge unahusu kutojumusihwa kwa ada ya ya hazina ya kukarabati barabara kwani kesi imewasilishwa mahakamani juu ya suala hilo.

Kulingana na Magavana, kaunti zina haki ya kupata ada hiyo ikizingatiwa kwamba zinajenga barabara na ni hazina ya ada ya mafuta ambayo hutoa fedha hizo.

Mkutano keshokutwa Ijumaa unatarajiwa kuchukua msimamo wa pamoja ikizingatiwa kwamba baadhi ya masuala yamejadiliwa katika kongamano la magavana hao ambalo ni asasi ya juu zaidi ya kufanya maamuzi.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article