Magari ya kushoto yapigwa marufuku nchini Kenya kuanzia Januari mwaka ujao

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirika la ukadiriaji ubora wa bidhaa nchini KEBS limetoa masharti mapya kwa wanaoagiza magari makuukuu nchini kuanzia tarehe moja mwezi ujao.

Kulingana na sheria hizo ni magari yanayoendeshwa mwa mkono wa kulia pekee yataruhusiwa nchini.

Pia ni magari yaliyotengezwa kuanzia Januari mosi mwkaa 2017 yataruhusiwa kuingia nchini.

Sheria za Kenya zinaruhusu magari yasiyozidi miaka minane kuingizwa nchini.

Hata hivyo magari ya ambulansi,zimamoto,magari ya miradi ya serikali yanaruhusiwa kuwa zaidiya miaka minane.

Magari ya kutoka mataifa ya Japan,muungano wa Uimarati,Uingereza,Thailand,Singapore, na Afrika Kusini ni lazima yaandamane na cheti cha ubora na ukaguzi.

Magari makuukuu ndio mengi humu nchini yakiwa asilimia 85 mengi yakitoka Japan.

Kenya huagiza magari 90,000 kila mwaka kutoka nje ya nchi.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article