Msanifu wa mitindo ya mavazi ambaye alishona nguo ambayo Priscilla Ojo alivaa wakati wa kupigwa picha za kabla ya harusi yake na Jux nchini Nigeria ametoa onyo kali kwa mafundi wa nguo.
Mtaalamu huyo kwa jina Lasosa, ambaye alishona pia nguo alizovaa Jux amesema kwamba yuko tayari kumshtaki yeyote ambaye hatachukuliwa kwa uzito onyo lake.
Anasema anamiliki haki zote za mavazi hayo na kwamba alitumia muda wake mwingi pamoja na juhudi katika kuyatengeneza na hivyo mitindo hiyo haifai kuigwa.
Priscy na Juma Jux wanaendelea kuzindua picha za kabla ya harusi ambazo walisema zitahusisha mavazi matano tofauti na ni mavazi yao ya pili yaliyovutia wengi mitandaoni.
Lasosa aliundia wapenzi hao nguo za mvuto wa hali ya juu ya rangi ya beji na kahawia.
Alitoa onyo hilo wakati wa mahojiano na Asoebi Styles jukwaa la mitandaoni ambalo huangazia pakubwa mitindo ya mavazi na hafla nchini Tanzania.
Lasosa anasema mitindo hiyo ni ya Priscilla na Juma Jux pekee na ni marufuku kwa yeyote kuiga.
“Mavazi haya niliyaunda kwa ajili ya wawili hawa pekee na ina maana kwamba tuna haki zote za mavazi haya.” alisema Lasosa.
Juma Jux yuko nchini Nigeria kwa ajili ya awamu ya huko ya ndoa yake na Priscilla mzaliwa wa Nigeria baada ya kukamilisha hafla tatu za ndoa hiyo nchini Tanzania.