Maeneo zaidi ya utawala yabuniwa Makueni kuboresha utoaji huduma

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali imebuni maeneo zaidi ya utawala katika kaunti ya Makueni katika hatua inayolenga kupeleka huduma karibu na raia. 

Maeneo yaliyobuniwa na kuwekwa katika gazeti rasmi la serikali ni pamoja na kaunti ndogo moja, divisheni 4, kata 28 na kata ndogo 48.

“Maeneo mapya ya utawala pia yataimarisha usalama, utaratibu wa umma, na utekelezaji sheria ili kubuni mazingira mwafaka ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi,” alisema Waziri wa Usalama wa Taifa Prof. Kithure Kindiki kufuatia kubuniwa kwa maeneo hayo.

“Inatarajiwa kwamba uwezo uliopanuliwa wa utekelezaji sheria utakabiliana na visa vya uharibifu wa miundombinu muhimu hasa reli, pombe haramu, ubakaji, kujiua na migogoro kati ya binadamu na wanyama pori.”

Katika mji wa Kiambu, Waziri Kindiki pia amezindua kaunti ndogo ya Kiambu na Teresia Mburu kutawazwa kama Naibu Kaunti Kamishna wa kwanza wa kaunti ndogo hiyo.

Share This Article