Maeneo mengi nchini yakosa nguvu za umeme

Tom Mathinji
1 Min Read

Kampuni ya usambazaji nguvu za umeme ya Kenya Power, imetangza kuwa maeneo mengi hapa nchini hayana nguvu za umeme kutokana na  kile ilichotaja kuwa hitilafu katika mifumo yao ya kimitambo.

Kupitia kwa taarifa katika mtandao wa X, kampuni hiyo ilisema hitilafu hiyo ilitokea saa kumi na moja Alhamisi jioni, ikisema juhudi zinatekelezwa kushughulikia hali hiyo.

“Mwendo wa saa kumi na moja na dakika 40 saa za Afrika Mashariki, Alhamisi Mei, 2, 2024, tulikumbwa na hitilafu za kimitambo na hivyo kusababisha kupotea kwa umeme katika sehemu nyingi za nchi,” ilisema taarifa hiyo.

Aidha katika taarifa hiyo, kampuni hiyo ilisema,” Tunasikitikia hali hiyo na tunawasihi wateja wetu kuwa watulivu huku tukijitahidi kurejesha hali kawaida haraka iwezekanavyo,”.

Iliahidi kutoa habari zaidi kuhusu hali hiyo katika muda wa masaa mawili.

TAGGED:
Share This Article