Maeneo kadhaa nchini kushuhudia mvua kubwa

Tom Mathinji
1 Min Read

Idara ya utabiri wa hali ya hewa imetoa tahadhari ya mvua kubwa katika maeneo kadhaa ya humu nchini.

Mvua ya rasharasha inatarajiwa katika maeneo ya Magharibi, kusini mwa Rift Valley, eneo la ziwa Victoria, Nyanda za juu kati mwa nchi, nyanda za chini kusini na kaskazini magharibi mwa nchi.

Baadhi ya sehemu henda zikapokea mvua kubwa hivyo wananchi wametakiwa kuwa macho kuhakikisha wako salama.

Kando na mvua, viwango vya juu vya joto wakati wa mchana vya zaidi ya nyuzi 30 vinatarajiwa katika kaunti kadhaa ikiwa ni pamoja na Turkana, Samburu, Marsabit, Mandera, Wajir, Isiolo, Garissa, Tana River, Lamu, Kilifi, Mombasa, Kwale, Taita Taveta, Kajiado, Makueni, Kitui, Laikipia, Baringo, Pokot Magharibi, Bungoma, Kakamega na Busia.

Wakazi wa kaunti hizo wametakiwa kuchukua tahadhari kuepuka athari za kiwango cha juu cha joto.

Wakati huohuo viwango vya joto vya chini vya hadi nyuzi 10 vinatarajiwa nyakati za usiku katika kaunti za Nyeri, Laikipia na Murang’a hivyo wakazi wa kaunti hizo wametakiwa kujistili ipasavyo nyakati za usiku.

Website |  + posts
Share This Article