Mwimbaji Madonna amesema kupitia taarifa kwamba anaendelea kupata nafuu baada ya kuugua na kulazwa hospitalini.
Kwenye taarifa hiyo yake ya kwanza tangu alipolazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi, Madonna alisema alijiwa na mawazo mawili alipoamka na kujipata kwenye kitanda hospitalini. Kwanza, aliwaza kuhusu watoto wake na pili aliwaza kuhusu kuwakatisha tamaa mashabiki ambao tayari walikuwa wamenunua tiketi za matamasha yake.
Madonna alilazimika kuahirisha ziara yake ya kikazi iliyokuwa imepangiwa kuanza Julai 15, 2023.
Anasema kwa sasa anaangazia afya yake lakini akahakikishia mashabiki wake kwamba atakuwa nao punde baada ya kupona na kupata nguvu.
Usimamizi wake unapanga kwamba aanze ziara yake ya Ulaya Oktoba 14 mjini London jinsi ilivyokuwa imepangwa awali na matamasha mengine yote ambayo yalikuwa yaandaliwe kabla ya hapo yatatafutiwa tarehe mpya baadaye.