Madaktari wa meno walalamikia ongezeko la madaktari bandia

Aidha, Madaktari hao wamelitaka Baraza la Kitaifa la Madaktari (KMPDC) kuwashirikisha katika uandaaji wa kanuni mpya za taaluma hiyo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha Madaktari wa Meno ( KDA) kimetishia kuitisha mgomo wa kitaifa kulalamikia ongezeko la wataalam bandia katika sekta hiyo humu nchini.

Wakizungumza na wanahabari jana Alhamisi, madaktari hao walielezea kutamaushwa kwao kutokana na hatua ya Baraza la Kitaifa la Madaktari (KMPDC) kushindwa kudhibiti sekta hiyo kikamilifu.

Pia wanataka kufutiliwa mbali kwa kanuni za kusimamia taaluma hiyo zilizochapishwa na madaktari wote bandia kupokonywa leseni.

Aidha, madaktari hao wametaka kushirikishwa katika uandaaji wa kanuni mpya za taaluma hiyo na KMPDC.

Madaktari hao pia wamesema hospitali nyingi za umma na za kaunti hazina wataalam wa kutosha wa meno na kupendekeza kuajiriwa kwa madaktari zaidi.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article