Madaktari kuandamana Jumanne kulalamikia hali ya afya nchini

Martin Mwanje
1 Min Read

Madaktari wanasema watafanya maandamano ya amani kesho Jumanne kulalamikia hali ya afya nchini.

“Tuko tayari kuandamana siku ya Jumanne. Kesho ndio siku. Ni kwa ajili ya taifa zima siyo madaktari pekee yao,” wamesema madaktari hao kupitia chama chao cha KMPDU kinachoongozwa na Katibu Mkuu Davji Atellah.

“Hii ni kuwataarifu wanachama na umma kwamba madaktari watafanya maandamano ya amani kulalamikia hali ya afya nchini Kenya.”

Madaktari kupitia chama chao cha KMPDU wamekuwa wakilalamikia kucheleweshwa kwa mishahara yao, hali wanayosema imefanya iwe vigumu kwao kujikimu kimaisha.

Aidha wanalalamikia mazingira mabovu ya utendakazi hususan ukosefu wa vifaa tiba na miundombinu muhimu inayohitajika ili kuimarisha utoaji huduma kwa wagonjwa kote nchini.

Chini ya katiba ya mwaka 2010, afya ni jukumu lililogatuliwa na sasa linasimamiwa na serikali za kaunti.

 

 

 

Share This Article