Mshukiwa mkuu katika vifo vya mamia ya watu eneo la Shakahola Paul Mackenzie na washirika wengine 29, wanatarajiwa kubaini hatima yao leo Jumatatu wakati wa kusikizwa kwa kesi yao na mahakama ya Mombasa.
Mackenzie amekuwa kizimbani tangu mwezi Aprili mwaka huu kwa madai ya kusababisha vifo vya watu zaidi ya 400 waliokuwa washirika wa kanisa lake la Goodlife International kupitia kwa mafunzo ya imani potovu.
Mamia ya watu wengine wanadaiwa kupotoshwa kupitia kwa mahubiri potovu katika kanisa hilo la Mackenzie.