Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 20 itawaalika Ethiopia katika uwanja wa Ulinzi Complex kuanzia saa tisa alasiri, katika raundi ya pili ya marudio kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026.
Kenya na Ethiopia ziliambulia sare ya bao moja katika duru ya kwanza mjini Adis Ababa wiki iliyopita.
Mshindi wa mechi ya leo atamenyana na Tanzania Februari mwaka ujao katika raundi ya tatu.