Maandalizi ya siku ya wafugaji wa ng’ombe wa maziwa Meru yaendelea

Marion Bosire
1 Min Read

Maandalizi ya siku ya wafugaji wa ng’ombe wa maziwa katika kaunti ya Meru yanaendelea na duru zinaarifu kwamba yanakaribia kukamilika.

Rais William Ruto anatarajiwa kuhudhuria.

Waandalizi wa hafla hiyo ya kesho itakayofanyika katika uwanja wa maonyesho wa Meru walionekana wakiweka vifaa kama hema, viti na viwambo katika eneo la tukio.

Akizungumza alipozuru uwanja wa maonyesho wa Meru leo, mkurugenzi mtendaji wa chama cha wafugaji wa ng’ombe wa maziwa huko Meru Kenneth Gitonga alisema kwamba wafugaji zaidi ya elfu 45 wanatarajiwa kuhudhuria.

Alisema hafla hiyo inalenga kuhamasisha wafugaji hao kuhusu njia bora za kutekeleza kazi zao na kutunza ng’ombe wa maziwa ili kuongeza kiwango cha maziwa.

Gitonga alisema wakulima hao wafugaji wa ng’ombe wa maziwa wanatarajia kwamba rais William Ruto atatekeleza ahadi aliyotoa mwaka jana ya kuwatengea shilingi milioni 100 za kujenga kiwanda cha chakula cha mifugo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *