Morocco itaandaa makala ya 35 ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika AFCON, kati ya Disemba 21 mwaka huu na Januari 18 mwakani.
Viwanja kadhaa kati ya tisa vilivyotengewa kuandaa michuano hiyo tayari vimekamilika huku ukarabati wa vingine vichache ukiwa ukingoni.
Uwanja wa Marrakech ulio mashariki mwa Morocco unakaribia kukamilika, wakati nyuga kama vile Prince Moulay Abdellah mjini Rabat na Agadir zikiwa tayari kwa mashindano.
Ukakarabati ambao umekuwa ukifanyiwa viwanja ulilenga kuongeza idadi, na utanywa upya baada ya fainali za AFCON kwa kipute cha kombe la Dunia mwaka 2030.
Miundo mbinu pia imeboreshwa ikiwemo barabara, reli ya kisasa na usafiri wa angani ili kufanikisha fainali za AFCON.
Morocco inaandaa AFCON kwa mara ya pili na ya kwanza tangu mwaka 1988.