Maafisa wawili wa polisi wanaofanya kazi katika kampuni ya Kenya Power, Ofisi ya Kanda ya Pwani wamekamatwa kwa madai ya kuitisha hongo ya shilingi 100, 000 kutoka kwa mlalamikaji.
Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC inasema maafisa waliokamatwa Inspekta Benjamin Ochieng na koplo Said Bakari.
Washukiwa wanadaiwa kuitisha hongo kutoka kwa mlalamikaji baada ya kumtuhumu kwa kujiunganishia umeme kinyume cha sheria katika makazi yake huko Bombolulu.
Maafisa hao wakidaiwa kuitisha mlungula ili kutomchunguza mlalamikaji na kuchukua hatua ya kisheria dhidi yake.
Baada ya kupokea ripoti kuhusu tukio hilo, EACC ilianzisha uchunguzi kubaini madai hayo.
Maafisa walijipata pabaya Agosti 24 walipomsindikiza mlalamikaji kwenye benki ili kukabidhiwa kitita cha hongo hiyo. Following a report on the alleged bribery demand, EACC commenced investigations to verify the allegations.
Nao walikamatwa mkabala wa benki ya DTB baada ya kupokea hongo ya shilingi 50,000 kutoka kwa mlalamikaji.
Washukiwa waliandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Central na kisha kuachuliliwa kwa dhamana ya shilingi 30,000 pesa taslimu wakati uchunguzi ukiendelea.