Maafisa wapya wa FKF wakutana na Rais wa FIFA

Dismas Otuke
0 Min Read

Rais wa FKF Hussein Mohammed pamoja na naibu wake McDonald Mariga walikutana na Rais wa shirikisho la kandanda ulimwenguni, Gianni Infantino, jana usiku nchini Morocco.

Hussein na Mariga walikuwa wakihudhuria tuzo za wachezaji na makocha bora wa mwaka zilizoandaliwa mjini Marrakech nchini Morocco.

Ilikuwa mara ya kwanza kwao kukutana na kinara wa FIFA, tangu wachaguliwe kuongoza kandanda nchini baada ya kutimuliwa kwa Nick Mwendwa na washirika wake.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *