Tume ya Maadili na kukabiliana na ufisadi, imewakamata maafisa wanne wa polisi kwa madai ya kuchukua hongo katika barabara ya Embu-Siakago.
Wanne hao Inspekta Sammy Cherogony, kopro Maurice Mwakachora, konstebo Fozia Hallake na konstabo Adan Mohamed, walinaswa baada ya uchunguzi kufanywa kufuatia malalamishi kutoka kwa umma.
Kulingana na EACC, maafisa hao wa polisi walikuwa wakichungzwa kwa siku kadhaa, wakipokea mlungula kutoka kwa waendeshaji magari na wananchi.
Maafisa hao walipelekwa katika makao makuu ya EACC, kabla ya kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilimani wakisubiri kufikishwa mahakamani.