Maafisa wanne wakuu wa polisi nchini Uganda wamewekewa vikwazo vya kusafiri nchini Marekani, kutokana na kuhusika kwao katika visa vya ukiukaji haki za kibinadamu.
Mathew Miller Msemaji wa idara ya marekani amewataja watatu hao kama Bob Kagarura, Kamanda wa zamani wa polisi ,kamanda wa zamani wa polisi katika wilaya ya Mitanya Alex Mwine, na naibu Mkurugenzi wa uchunguzi wa kesi za jinai Elly Womanya.
Maafisa hao pamoja na familia zao wamewekewa vikwazo vya kusafiri kwenda Marekani.
Orodha hiyo pia inamjumuisha aliyekuwa kamishna mkuu wa polisi Kale Kayihura,Abel Kanduho na kamishna mkuu wa Magereza Johnson Byabashaija.
Marekani na Uingereza zilikuwa pia zimewawekea vikwazo vya usafiri Spika wa bunge la Uganda Anita Among na mawaziri wote sasa na wale wa zamani kwa madai ya kujihusisha katika ufisadi na pia visa vya ukiukaji haki za binadamu.