Maafisa wafisadi serikalini mashakani

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto amesema atawakabili vilvyo maafisa wa serikali wanaojihusisha na ufisadi, akidokeza hatarusu rasilimali za umma zikitumika visivyo.

Akizungumza siku ya Ijumaa wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya Mashujaa katika kaunti ya Kericho, Rais alisema serikali yake italinda rasilimali za umma kwa vyovyote vile.

“Tayari nimetangaza kwamba, hatutavumilia ufisadi hapa nchini. Wale watakaojihusisha, tutawakabili vilivyo,” alionya Rais Ruto.

Katika onyo lake kali, kiongozi wa nchi alisema hivi karibuni wakenya wataanza kuona matunda kutokana na vita dhidi ya ufisadi, akisema wafisadi wote watabeba msalaba wao.

“Natoa ahadi kwamba nitalinda pesa zote za serikali, ambazo mmkusanya kupitia ushuru, na zitatumika vizuri. Pesa hizo zitalindwa na wafisadi hawataweza kuzifuja,”aliongeza rais Ruto.

Aliwahimiza na kuwahakikishia wakenya kwamba serikali yake haitapoteza mwelekeo katika kuhakikisha ushuru wa wakenya unatumiwa ipasavyo ili kukuza uchumi wa nchi.

Share This Article