Maafisa wa usalama, raia wanaojituma katika vita dhidi ya uhalifu kuzawadiwa

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali kuu itaanzisha mpango wa kuwazadia fedha maafisa wanaojituma kazini na raia wanaosaidia katika juhudi za kuwakamata wapangaji wakuu, watekelezaji na wawezaji wa uhalifu  nchini. 

Waziri wa Usalama wa Kitaifa Prof. Kithure Kindiki amesema picha za washukiwa wa uovu huo zitachapishwa kote nchini mwakani.

Kindiki alisema hayo akiwa eneo la Posta, kaunti ya Laikipia leo Ijumaa aliposimamia kurejeshwa kwa ng’ombe walioibwa.

Maafisa wa usalama, viongozi wa eneo hilo na vijana ambao jitihada zao zilisaidia katika kupatikana kwa ng’ombe hao walizawadiwa wakati wa hafla hiyo.

Waziri alisema ili kuangamiza miundombinu ya wezi wa ng’ombe na wawezeshaji wao, serikali inaendeleza vita dhidi ya uhalifu na wanaoutekeleza, kuuwezesha na kufaidi nao kwa kuhakikisha wanagharimia mno vitendo vyao.

Eneo la kaskazini mwa nchi miaka iliyopita limeshuhudia kukithiri kwa wizi wa ng’ombe na Waziri Kindiki ameahidi kufanya kila awezalo kukomesha uovu huo.

Share This Article