LSK kuandaa kikao cha kila mwaka Kwale

Martin Mwanje
1 Min Read

Kikao cha kila mwaka kinachoandaliwa na Chama cha Wanasheria nchini, LSK kimeanza leo Jumanne katika eneo la Diani, kaunti ya Kwale. 

Maudhui ya kikao hicho cha siku tatu ni “Uwezeshaji wa Uanasheria Bora; Maongozi Bora na Utawala wa Sheria kwa ajili ya Maendeleo Endelevu.

Jaji Mkuu Martha Koome atafungua rasmi kikao hicho Alhamisi wiki hii.

Kikao hicho kinaandaliwa wakati LSK imekuwa mstari wa mbele kupinga ukandamizaji wa waandamanaji ulioshuhudiwa wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z humu nchini.

Aidha, chama hicho kinachoongozwa na Faith Odhiambo kimelalamikia visa vilivyokithiri vya watu kutekwa nyara katika siku za hivi karibuni, ambavyo kinasema ni pigo kwa mafao yaliyopatikana kutokana na kupitishwa kwa katiba ya mwaka 2010.

Haya, pamoja na utenda kazi wa idara ya mahakama ni baadhi ya masuala yanayotarajiwa kupewa kipaumbele wakati wa kikao hicho kitakachohudhuriwa na wanasheria kutoka sehemu mbalimbali nchini.

 

 

 

TAGGED:
Share This Article