Lori lililokuwa na watu 10 lasombwa na mafuriko kaunti ya Makueni

Tom Mathinji
1 Min Read
Lori lasombwa na mafuriko kaunti ya Makueni.

Lori  lililokuwa na watu 10, limesombwa na mafuriko lilipokuwa likijaribu kuvuka mto kwa Muswii, uliokuwa umefurika katika eneo la Kasikeu area, Sultan Hamud ikaunti ya Makueni.

Lori hilo pia lilikuwa limebeba mchanga.

Shirika la msalaba mwekundu kupitia mtandao wa X, umedokeza kuwa maafisa wake wamefika katika eneo la mkasa, kwa shughuli ya uokoaji.

Hadi kufikia sasa watu saba  wameokolewa na kupelekwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Sultan Hamud kwa matibabu.

Maeneo mengi hapa nchini yanashuhudia mvua kubwa ambayo imesababisha mafuriko.

Rais William Ruto amewaagiza maafisa wa vikosi vya ulinzi na wale wa huduma ya vijana kwa taifa NYS, kusaidia katika shughuli ya kuwahudumia wanaothirika na mafuriko.

TAGGED:
Share This Article