Lokedi atwaa nafasi ya Kosgei katika timu ya Olimpiki ya marathon

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa New York Marathon mwaka 2022 Sharon Lokedi, ametwaa nafasi ya Brigid Kosgei katika timu ya mbio za marathon katika makala ya 31 ya michezo ya Olimpiki.

Lokedi aliyekuwa mwanariadha wa akiba amejumuishwa katika kikosi baada ya Kosgei, ambaye ni mshikilizi wa zamani wa rekodi ya Dunia ya  marathon kujeruhiwa akiwa mazoezini.

Lokedi aliye na umri wa miaa 30 na ambaye ni mshindi wa nishani ya fedha katika mbio za Boston marathon mwaka huu, anajiunga na bingwa mtetezi Peres Jepchirchir na bingwa mara mbili wa Boston marathon Hellen Obiri katika kikosi cha mbio za kilomita 42.

Marathon ya wanawake litakuwa shindano la mwisho Agosti 11 katika michezo ya Olimpiki .

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *