Lisu alalamikia matumizi ya vyombo vya dola kukandamiza upinzani Tanzania

Dismas Otuke
1 Min Read

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lisu amelalamikia matumizi ya vyombo vya dola na serikali tawala nchini humo kukandamiza upinzani.

Lisu ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema amesema kuwa nchi hiyo ingali nyuma kuwakomboa raia wake.

Akigusia visa vya utekaji nyara na mauaji ya wanasiasa wa upinzani, Lisu ameishutumu serikali kwa kile alichokitaja kuwa matumizi mabaya ya maafisa wa polisi na pia kukandamizia demokrasia.

Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwaka ujao ambapo Rais Samia Suluhu Hassan atawania kuchaguliwa kwa mara ya kwanza.

Suluhu aliyekuwa Makamu wa Rais alitwaa mamlaka Machi 19 mwaka 2021 kufuatia kifo cha Rais John Magufuli kilichotokana na matatizo ya moyo punde baada ya kushinda muhula wa pili.

Website |  + posts
Share This Article