Ligi Kuu ya Kenya yaingia mzunguko wa 24

Dismas Otuke
2 Min Read

Kinyang’anyiro cha Ubingwa wa Ligi Kuu ya FKF kinaingia raundi ya 24 mwishoni mwa juma hili .

Jumamosi City Stars watawaalika Bidco United ugani Kenyatta kaunti ya machakos saa saba mchana, kabla ya Batoto ba Mungu- Sofapaka kupimana ubabe na Muranga Seal saa kumi jioni kiwarani humo.

Mtanange wa mwisho utapepetwa pwani wenyeji Bandari wakizichapa dhidi ya viongozi wa jedwali Kogalo-Gor Mahia.

Siku ya jumapili itakuwa zamu ya Postar Rangers kutesa nyasi za uwanja wa Police Sacco dhidi ya vijana wa Kariobangi Sharks saa saba, kisha saa kumi jioni Polisi wakamenyane na Muhoroni.

Wanamvinyo Tusker watakuwa na kibatrua dhidi ya Ingwe .

Mchuano huo ulistahili kugaragazwa nyumbani kwa Tusker, lakini ukahamishwa kwa sababu ya hali mbaya ya uwanja huo.

Mwendo wa sa kumi jioni, macho yote yataangalia magharibi ya nchi wakati Bana be ingo-Kakamega Homeboyz watakapojihami dhidi ya wanajeshi-Ulinzi Stars huko Mumias Complex.

Kilomita chache kutoka pale, litakuwa pambano kali ugani Sudi baina ya wenyeji Nzoia na Talanta.

Wanasukari –Nzoia, wana burura mkia kwenye ligi na wamo kwenye hatari kubwa ya kushushwa daraja, hivyo, ngarambe hii itakuwa ya kufa kupona kwa lengo la kujinasua.

Raundi ya 24 ya Ligi ya KPL ilianza Ijumaa Ijumaa KCB wakiibwaga Shabana FC mabao 3-2 na kudidimiza matumaini ya Shabana kusalia ligini Msimu ujao.

TAGGED:
Share This Article