Lagat, ajiondoa afisini kwa muda kupisha uchunguzi wa mauaji ya Ojwang’

Lagat amesemaamejiondoa ili kupisha uchunguzi wa kina kuhusiana na mauaji ya Ojwang

Dismas Otuke
1 Min Read

Naibu Inspekta Jenerali Mkuu wa Polisi Eliud Lagat, amejiondoa afisini kwa muda kuruhusu uchunguzi wa mauji ya Mwanablogu Albert Ojwang,  akiwa kwenye korokoro ya polisi.

Kwenye taarifa iliyotolewa Jumatatu jioni Lagat, amesema hatua hiyo ni ya nia njema kuhusiana na majukumu yake.

Lagat amesema amejiondoa ili kupisha uchunguzi wa kina kuhusiana na mauaji ya Ojwang .

Lagat ameongeza kuwa majukumu yake yatatekelezwa na Naibu wake hadi pale uchunguzi utakapokamilika.

Aidha ameahidi kusaidia katika uchunguzi ya mauaji ya Ojwang, na kutoa rambirambi kwa familia .

Website |  + posts
Share This Article