Lady Jaydee kuzindua kitabu kumhusu

Hatua hii ni sehemu ya shughuli mbali mbali ambazo amepanga mwimbaji huyo, anapoadhimisha miaka 25 katika tasnia ya muziki.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa muda mrefu wa Tanzania Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee ametangaza ujio wa kitabu kinachohadithia safari yake katika muziki.

Alitumia akaunti yake ya Instagram kutoa tangazo hilo ambap aliandika, “Nitakua ninazindua kitabu kuhusiana na safari yangu ya miaka 25.”

Hatua hii ni sehemu ya shughuli mbali mbali ambazo amepanga mwimbaji huyo, anapoadhimisha miaka 25 katika tasnia ya muziki nchini Tanzania.

Kulingana naye, kitabu hicho kitaelezea kwa kina alipotoka, mambo ambayo ameyaona, aliyoyapitia, alichojifunza, alipokwama na alipofanikiwa.

Shughuli za kuadhimisha miaka 25 ya Lady Jaydee zitaendelea kwa juma zima kati ya Juni 9 na 13 mwaka huu wa 2025.

Website |  + posts
Share This Article