KURA yafunga barabara ya UN Avenue mtaani Runda

Dismas Otuke
0 Min Read

Mamlaka ya barabara za mijini (KURA) imetangaza kufunga barabara ya UN-Avenue,mtaani Runda kutokana na mafuriko yaliyosababisha na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa Jumapili.

Maeneo yaliyoathiriwa ni karibu na mzunguko wa barabara ya Ruaka na Magnolia close.

Waendeshaji magari wanaotumia barabara hiyo wameshauriwa kutiumia barabara mbadala.

TAGGED:
Share This Article