Kura ya maoni ya TIFA: Waziri Kindiki apendekezwa kumrithi Gachagua

Martin Mwanje
1 Min Read
Prof. Kithure Kindiki, kuapishwa kuwa Naibu Rais Ijumaa.

Utafiti wa hivi punde uliofanywa na kampuni ya TIFA unaonyesha kuwa Wakenya wengi wanataka Waziri wa Usalama wa Taifa Prof. Kithure Kindiki kutajwa kama Naibu Rais ikiwa Rigathi Gachagua ataondolewa kwenye wadhifa huo. 

Kulingana na utafiti huo, asilimia 37 ya Wakenya wanataka Prof. Kithure Kindiki kurithi wadhifa huo huku asilimia 5 wakitaka ukabidhiwa ama Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi au mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro.

Asilimia 3 ya waliohojiwa walipendekeza mikoba ya wadhifa huo ikabidhiwe Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru huku asilimia 2 ikipendekeza wadhifa huo kukabidhiwa Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga.

Utafiti huo ulifanywa kati ya Oktoba 1-4, 2024 huku watu 1,892 wakihojiwa katika kaunti zote 47 kote nchini.

Share This Article