KUPPET yasitisha mgomo wa Walimu baada ya kuafikiana na TSC

Dismas Otuke
1 Min Read
Mgomo wa walimu wa KUPPET wasimamiswa na mahakama.

Walimu kote nchini wanatarijiwa kurejea shuleni kesho Jumanne, baada ya Muungano wa walimu wa shule za sekondari na vyuo KUPPET, kutangaza kusitisha mgomo Jumatatu jioni.

Mgomo huo umesitishwa baada ya KUPPET na tume ya kuwajiri walimu TSC kuafikiana .

Katibu Mkuu wa KUPPET Akelo Misori ametangaza kusitisha mgomo huo uliokuwa umedumu kwa wiki moja iliyopita.

Haya yanajiri wakati ambapo wanafunzi wa shule za sekondari walikuwa wameamrishwa kurejea nyumbani kutokana na mgomo ambao ulikuwa umeanza wiki ya pili siku ya Jumatatu.

Misori ameongeza kuwa watatoa taarifa zaidi kulingana na uamuzi wa kesi itakayotolewa hukumu siku ya Alhamisi wiki hii.

Afisa Mkuu mtendaji wa tume ya TSC Nancy Macharia, amesema pande hizo mbili zimeafikiana kutafuta mbinu mbadala ya kusuluhisha mzozo huo.

Macharia ameongeza kuwa marupurupu ya nyongeza a mishahara ya walimu ililipwa pamoja na mishahara ya mwezi Agosti.

Walimu walitaka miongoni mwa matakwa ikiwemo utekelezaji kikamilifu wa nyongeza ya mshahara mwaka 2021-2025,kupandishwa vyeo kwa walimu 130,000 miongoni mwa masharti mengine.

TAGGED:
Share This Article