KTB kuwawezesha vijana kujinufaisha na biashara ya utalii

Martin Mwanje
1 Min Read

Bodi ya Utalii Nchini, KTB inasema itajenga uwezo wa vijana kujitosa katika biashara ya utalii katika kaunti kwa lengo la kuongeza ujuzi wao katika sekta hiyo.  

Mwenyekiti wa KTB Francis Gichaba amedokeza kuwa vijana kadhaa katika maeneo mbalimbali wanaoendesha shughuli za utalii hawana ujuzi na uelewa unaohitajika kutoa huduma bora za kuwavutia watalii. 

“Kama shirika la kunadi utalii, hii ni moja ya sehemu tutakazoangazia hasa wakati tukiboresha uhusiano wetu na serikali za kaunti katika kutambua fursa zitakazochochea utalii katika kaunti hizo”, alisema Gichaba.

Akizungumza pembezoni mwa tamasha zilizomalisika za Utalii na Utamaduni za Turkana mjini Lodwar, Gichaba alisema biashara ya utalii ni moja ya nguzo muhimu za kiuchumi nchini ambazo zina athari ya moja kwa moja kuanzia viwango vya mashinani. 

 

Share This Article