KQ yarejesha safari za Nairobi hadi Eldoret asema Murkomen

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa barabara na uchukuzi Kipchumba Murkomen, ametangaza kurejeshwa kwa safari za ndege za shirika la Kenya Airways(KQ) kutoka Nairobi hadi Eldoret.

Kwa mujibu wa Murkomen, uwanja wa Eldoret utakuwa kituo cha 44 cha shirika hilo duniani na kinalenga kuboresha biashara na usafiri wa haraka wa eneo hilo.

Aliyasema haya katika uwanja wa ndege wa Eldoret wakati wa uzinduzi wa shuguli hiyo.

Aliongeza kuwa barabara ya uwanja huo itarefushwa hadi kilomita 4.2 kupitia bajeti ya mwaka ujao huku akimwomba Afisa Mkuu Mtendaji wa KQ Allan Kilavuka kupunguza nauli ili kuwavutia abiria wengi.

Hatua hii inajiri miaka 10 tangu shirika hilo likatize safari za Eldoret na nimojawapo ya mipango ya serikali ya kuimarisha na kurahisisha usafiri wa ndege kote nchini, miezi kadhaa baada ya kurejeshwa kwa safari za ndege za hadi Kakamega.

Shirika hilo litafanya safari tano kila juma huku likilenga ongezeko la wasafiri.

Share This Article