KQ yaongeza safari mbili za ndege kutoka Nairobi hadi New York

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya ndege ya Kenya Airways maarufu kama KQ, imetangaza kuongeza safari mbii za kutoka Nairobi hadi New York kati ya Juni 15 na Septemba 28 mwaka huu.

Kulingana na taarifa ya KQ hatua hiyo inalenga kukidhi ongezeko la wasafiri katika msimu wa majira ya joto.

Idadi hiyo mpya itafikisha jumla ya safari 9 za KQ, wateja wakiwa na uhuru wa kuchagua kati ya ndege za asubuhi au jioni.

KQ ilianzisha safari za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi New York mwaka 2018.

Website |  + posts
Share This Article