Korea Kaskazini yaikwatua Marekani na kufuzu fainali ya Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Korea Kaskazini ilifuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia kwa akina dada chini ya umri wa miaka 17 baada ya kuwatema nje Marekani bao moja kwa bila.

Nusu fainali hiyo ya kwanza ilisakatwa jana usiku katika uwanja wa Cibao mjini San Dominqo katika Jamhuri ya Dominica.

Bao pekee na la ushindi kwa Korea Kaskazini lilipachikwa kuanko dakika ya 67 kupitia kwa Ro Un-Hyang.

Korea watashuka uwanjani Jumapili kwa fainali dhidi ya atakayeshinda nusu fainali ya pili kesho baina ya Uingereza na Uhispania.

Ni fainali ya pili mtawalia kwa Korea Kaskazini kufuzu baada ya kunyakua kombe la Dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20.

Share This Article