Jaji mkuu Martha Koome ameonya kwamba matamshi ya uchochezi na makundi ya wahuni yanapasa kukabiliwa vilivyo, akiyataja kuwa hatari kwa usalama huku nchi hii inapojiandaa akwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Koome aliyekariri kujitolea kwa Idara ya Mahakama kuhakikisha haki ya uchaguzi nchini Kenya, alisema teknolojia ibuka ni changamoto kubwa inayohitaji kushughulikiwa kwa dharura.
“Nahakikisha kujiolea kwa Idara ya Mahakama kuimarisha haki katika mfumo wa kiuchaguzi hapa nchini Kenya,” alisema Koome.
Jaji huyo Mkuu liyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kamati ya mpango wa shughuli za uchaguzi, itakayoshughulikia mizozo ya uchaguzi huku mahakama ya upeo ikipendekeza kuongezwa kwa jopo la majaji wa kusikiza kesi za mizozo ya uchaguzi kutoka majaji saba hadi tisa.
Suala la ufadhili pia lilitajwa kuwa muhimu kwa tume ya IEBC huku chguzi ndogo zikitarajiwa ambazo mkuu wa sheria Dorcas Oduor alitoa wito kwa idara ya mahakama iingilie kati baada ya kukamilika kwa muda wa siku tisini baada bunge kutangaza viti hivyo kuwa wazi.