Kongamano la 24 la kawaida la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), litaandaliwa leo mjini Arusha Tanzania huku likiwaleta pamoja viongozi kutoka mataifa yote manane wanachama.
Kongamano hilo itakuwa la kipekee huku EAC ikiadhimisha miaka 25 tangu ibuniwe mwaka 1999.
Baadhi ya masuala yanayotarajiwa kujadiliwa ni hali ya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mafanikio ya jumuiya hiyo tangu kubuniwa kwake, changamoto zilizopo katika utangamano wa jumuiya na suluhisho.
EAC inajumuisha mataifa manane ya Afrika Mashariki ambayo ni wanachama yakiwa:-Kenya, Uganda,Tanzania, Burundi,Rwanda,DR Congo, Somalia na Sudan Kusini.